29. Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako.
30. Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho!
31. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
32. Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo.
33. Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote.