Yn. 6:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng’ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia.

2. Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa.

3. Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.

4. Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu.

5. Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula?

6. Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda.

7. Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu.

8. Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,

9. Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?

Yn. 6