Yn. 3:3-9 Swahili Union Version (SUV)

3. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

6. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

8. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

9. Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya?

Yn. 3