Kwa milima nitalia na kulalama,Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo;Kwa sababu yameteketea, hata hapana apitaye,Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng’ombe;Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni,Wamekimbia, wamekwenda zao.