Yer. 5:29-31 Swahili Union Version (SUV)

29. Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?

30. Jambo la ajabu, la kuchukiza, limetokea katika nchi hii!

31. Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?

Yer. 5