Yer. 46:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Nani huyu ajiinuaye kama mto Nile,Ambaye maji yake yanajirusha kama mito?

8. Misri anajiinua kama mto Nile,Na maji yake yanajirusha kama mito;Asema, Nitajiinua, nitaifunikiza nchi;Nitauharibu mji na hao wakaao ndani yake.

9. Haya! Pandeni, enyi farasi;Jihimizeni, enyi magari ya vita;Mashujaa nao na watoke njeKushi na Puti, watumiao ngao;Nao Waludi, washikao uta na kuupeta.

10. Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi,Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake;Nao upanga utakula na kushiba,Utakunywa damu yao hata kukinai;Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yakeKatika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.

Yer. 46