Yer. 29:3-5 Swahili Union Version (SUV)

3. kwa mkono wa Elasa, mwana wa Shafani, na Gemaria, mwana wa Hilkia, (ambao Sedekia, mfalme wa Yuda, aliwatuma hata Babeli, kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli), kusema,

4. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, awaambia hivi watu wote waliochukuliwa mateka, niliowafanya wachukuliwe toka Yerusalemu mpaka Babeli;

5. Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake;

Yer. 29