1. Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, hapo mfalme Sedekia alipompelekea Pashuri, mwana wa Malkiya, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kusema,
2. Tafadhali utuulizie habari kwa BWANA; kwa maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda BWANA atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, ili aende zake akatuache.