Yer. 2:35-37 Swahili Union Version (SUV)

35. Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.

36. Mbona unatanga-tanga hivi upate kugeuza mwendo wako? Utaona haya kwa ajili ya Misri pia, kama ulivyoona haya kwa ajili ya Ashuru.

37. Hata kwake pia utatoka, na mikono yako juu ya kichwa chako; kwa maana BWANA amewakataa uliowakimbilia, wala hutafanikiwa katika hao.

Yer. 2