1. Tena neno la BWANA likanijia, kusema,
2. Wewe hutaoa mke, wala hutakuwa na wana wala binti mahali hapa.
3. Maana BWANA asema hivi, katika habari za wana, na katika habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na katika habari za mama zao waliowazaa, na katika habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;