1. Neno la BWANA lililomjia Yeremia, katika habari ya ukosefu wa mvua.
2. Yuda huomboleza,Na malango yake yamelegea;Wameketi chini wamevaa kaniki;Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.
3. Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji;Nao hufika visimani wasione maji;Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu;Wametahayarika na kufadhaika,Na kuvifunika vichwa vyao.
4. Kwa sababu ya nchi iliyopasuka,Kwa kuwa mvua haikunyesha katika nchi,Wenye kulima wametahayarika,Na kuvifunika vichwa vyao.
5. Naam, kulungu naye uwandani amezaa,Akamwacha mwanawe kwa kuwa hapana majani.