1. Neno la BWANA lililomjia Yeremia, katika habari ya ukosefu wa mvua.
2. Yuda huomboleza,Na malango yake yamelegea;Wameketi chini wamevaa kaniki;Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.
3. Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji;Nao hufika visimani wasione maji;Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu;Wametahayarika na kufadhaika,Na kuvifunika vichwa vyao.