15. Sikilizeni ninyi, kategeni masikio yenu; msifanye kiburi; maana BWANA amenena.
16. Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
17. Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa hali ya kufungwa.
18. Mwambie mfalme, na mama ya mfalme,Nyenyekeeni na kuketi chini;Kwa maana vilemba vyenu vimeshuka,naam, taji ya utukufu wenu.