12. Ameiumba dunia kwa uweza wake,Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake,Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
13. Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni,Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi;Huifanyia mvua umeme,Huutoa upepo katika hazina zake.
14. Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa;Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga;Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo,Wala hamna pumzi ndani yake.
15. Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu;Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.
16. Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;Na Israeli ni kabila ya urithi wake;BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
17. Haya! Kusanya bidhaa yako katika nchi, wewe ukaaye katika mazingiwa.