Yak. 1:9-14 Swahili Union Version (SUV)

9. Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;

10. bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.

11. Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

12. Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

13. Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

14. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

Yak. 1