15. BWANA ameziondoa hukumu zako,Amemtupa nje adui yako;Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yu katikati yako;Hutaogopa uovu tena.
16. Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.
17. BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;Atakushangilia kwa furaha kuu,Atakutuliza katika upendo wake,Atakufurahia kwa kuimba.
18. Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao.
19. Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote.