13. Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake.
14. Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu;I karibu, nayo inafanya haraka sana;Naam, sauti ya siku ya BWANA;Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
15. Siku ile ni siku ya ghadhabu,Siku ya fadhaa na dhiki,Siku ya uharibifu na ukiwa,Siku ya giza na utusitusi,Siku ya mawingu na giza kuu,
16. Siku ya tarumbeta na ya kamsa,Juu ya miji yenye maboma,Juu ya buruji zilizo ndefu sana.