Rum. 4:22-25 Swahili Union Version (SUV)

22. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

23. Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake;

24. bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;

25. ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

Rum. 4