20. Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
21. huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
22. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.
23. Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake;
24. bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;
25. ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.