10. Na tena anena,Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.
11. Na tena,Enyi Mataifa yote, msifuni Bwana;Enyi watu wote, mhimidini.
12. Na tena Isaya anena,Litakuwako shina la Yese,Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;Ndiye Mataifa watakayemtumaini.
13. Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
14. Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.