32. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
33. Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
34. Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?
35. Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena?