Omb. 2:3-7 Swahili Union Version (SUV)

3. Ameikata pembe yote ya IsraeliKatika hasira yake kali;Ameurudisha nyuma mkono wake wa kuumeMbele ya hao adui,Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao,Ulao pande zote.

4. Ameupinda upinde wake kama adui,Amesimama na mkono wake wa kuume kama mtesi;Naye amewaua hao woteWaliopendeza macho;Katika hema ya binti SayuniAmemimina kani yake kama moto.

5. Bwana amekuwa mfano wa adui,Amemmeza Israeli;Ameyameza majumba yake yote,Ameziharibu ngome zake;Tena amemzidishia binti YudaMatanga na maombolezo.

6. Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu,Kana kwamba ni ya bustani tu;Ameziharibu sikukuu zake;BWANA amezisahauzisha katika SayuniSikukuu za makini na sabato;Naye amewadharau mfalme na kuhaniKatika uchungu wa hasira yake.

7. Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake,Amepachukia patakatifu pake;Amezitia katika mikono ya hao aduiKuta za majumba yake;Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANAKama katika siku ya kusanyiko la makini.

Omb. 2