Omb. 1:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Yerusalemu amefanya dhambi sana;Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu;Wote waliomheshimu wanamdharau,Kwa sababu wameuona uchi wake;Naam, yeye anaugua,Na kujigeuza aende nyuma.

9. Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake;Hakukumbuka mwisho wake;Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu;Yeye hana mtu wa kumfariji;Tazama, BWANA, teso langu;Maana huyo adui amejitukuza.

10. Huyo mtesi amenyosha mkono wakeJuu ya matamaniko yake yote;Maana ameona ya kuwa makafiri wameingiaNdani ya patakatifu pake;Ambao kwa habari zao wewe uliamuruWasiingie katika kusanyiko lako.

11. Watu wake wote hupiga kite,Wanatafuta chakula;Wameyatoa matamaniko yao wapate chakulaCha kuihuisha nafsi;Ee BWANA, tazama, uangalie;Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.

12. Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia,Angalieni, mtazameKama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu,Niliyotendwa mimi,Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayoSiku ya hasira yake iwakayo.

Omb. 1