11. Watu wake wote hupiga kite,Wanatafuta chakula;Wameyatoa matamaniko yao wapate chakulaCha kuihuisha nafsi;Ee BWANA, tazama, uangalie;Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.
12. Je! Si kitu kwenu, enyi nyote mpitao njia,Angalieni, mtazameKama kuna majonzi yo yote mfano wa majonzi yangu,Niliyotendwa mimi,Ambayo BWANA amenihuzunisha kwa hayoSiku ya hasira yake iwakayo.
13. Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu,Nao umeishinda;Ametandika wavu aninase miguu,Amenirudisha nyuma;Amenifanya kuwa mtu wa pekee,Na mgonjwa mchana kutwa.
14. Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake;Hayo yameshikamana;Yamepanda juu shingoni mwangu;Amezikomesha nguvu zangu;