Neh. 7:63-65 Swahili Union Version (SUV)

63. Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.

64. Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.

65. Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.

Neh. 7