Neh. 3:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli.

2. Na baada yao wakajenga watu wa Yeriko. Na baada yao akajenga Zakuri, mwana wa Imri.

3. Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.

4. Na baada yao akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi. Na baada yao akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli. Na baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Baana.

5. Na baada yao wakafanyiza Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao.

Neh. 3