3. Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.
4. Magari ya vita yanafanya mshindo njiani,Yanasongana-songana katika njia kuu;Kuonekana kwake ni kama mienge,Yanakwenda upesi kama umeme.
5. Awakumbuka watu wake wenye heshima;Wanajikwaa katika mwendo wao;Wanafanya haraka waende ukutani;Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.
6. Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa.
7. Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao.
8. Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.