6. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
7. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
8. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
9. Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
10. Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi.