Mwa. 35:12-15 Swahili Union Version (SUV)

12. Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.

13. Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.

14. Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.

15. Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.

Mwa. 35