Mwa. 19:23-26 Swahili Union Version (SUV)

23. Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari.

24. Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA.

25. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.

26. Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi.

Mwa. 19