Mwa. 1:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

3. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

4. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.

5. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Mwa. 1