Mt. 9:22-24 Swahili Union Version (SUV)

22. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

23. Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,

24. akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.

Mt. 9