Mt. 8:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.

2. Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.

3. Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.

4. Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

5. Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

6. akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

7. Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

Mt. 8