31. Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32. Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.