Mt. 6:15-22 Swahili Union Version (SUV)

15. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

16. Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

17. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

18. ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

19. Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

20. bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

21. kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

22. Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.

Mt. 6