1. Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,
2. Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
3. Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema,Sauti ya mtu aliaye nyikani,Itengenezeni njia ya Bwana,Yanyosheni mapito yake.
4. Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.