Mt. 25:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

2. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.

3. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

4. bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

5. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

6. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

Mt. 25