Mt. 15:5-14 Swahili Union Version (SUV)

5. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,

6. basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

7. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,

8. Watu hawa huniheshimu kwa midomo;Ila mioyo yao iko mbali nami.

9. Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundishoYaliyo maagizo ya wanadamu.

10. Akawaita makutano akawaambia

11. Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.

12. Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?

13. Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.

14. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Mt. 15