35. Akawaagiza mkutano waketi chini;
36. akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
37. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.
38. Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila wanawake na watoto.
39. Akawaaga makutano, akapanda chomboni, akaenda pande za Magadani.