Mt. 13:53-56 Swahili Union Version (SUV)

53. Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake.

54. Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?

55. Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?

56. Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?

Mt. 13