Mt. 12:12-23 Swahili Union Version (SUV)

12. Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.

13. Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili.

14. Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.

15. Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,

16. akawakataza wasimdhihirishe;

17. ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

18. Tazama, mtumishi wangu niliyemteua;Mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye;Nitatia roho yangu juu yake,Naye atawatangazia Mataifa hukumu.

19. Hatateta wala hatapaza sauti yake;Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.

20. Mwanzi uliopondeka hatauvunja,Wala utambi utokao moshi hatauzima,Hata ailetapo hukumu ikashinda.

21. Na jina lake Mataifa watalitumainia.

22. Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.

23. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?

Mt. 12