7. Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia.
8. Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.
9. Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga.
10. Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha.
11. Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.
12. Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.
13. Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo.