Mk. 8:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali.

4. Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani?

5. Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba,

6. Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano.

7. Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia.

8. Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.

Mk. 8