Mk. 8:11-14 Swahili Union Version (SUV)

11. Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.

12. Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.

13. Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo.

14. Wakasahau kuchukua mikate, wala chomboni hawana ila mkate mmoja tu.

Mk. 8