5. Yesu akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye.
6. Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi.
7. Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.
8. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
9. Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.
10. Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.