31. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
32. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
33. Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
34. Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.