Mk. 12:25-27 Swahili Union Version (SUV)

25. Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.

26. Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?

27. Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.

Mk. 12