Mk. 11:5-8 Swahili Union Version (SUV)

5. Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwana-punda?

6. Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza, nao wakawaruhusu.

7. Wakamletea Yesu yule mwana-punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.

8. Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani.

Mk. 11