Mk. 10:50-52 Swahili Union Version (SUV)

50. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu.

51. Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona.

52. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.

Mk. 10