Mit. 8:12-18 Swahili Union Version (SUV)

12. Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu;Natafuta maarifa na busara.

13. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;Kiburi na majivuno, na njia mbovu,Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

14. Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi;Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.

15. Kwa msaada wangu wafalme humiliki,Na wakuu wanahukumu haki.

16. Kwa msaada wangu wakuu hutawala,Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.

17. Nawapenda wale wanipendao,Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

18. Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo, na haki pia.

Mit. 8